Breaking News

ZIFAHAMU NGUZO MBILI MUHIM KATIKA MAHUSIANO/NDOA YAKO

ZIFAHAMU NGUZO MBILI MUHIM KATIKA MAHUSIANO/NDOA YAKO

Bila shaka swala zima la mahusiano au ndoa siyo jambo geni kulisikia katika maisha yako,ni jambo ambalo umezaliwa umelikuta na utakufa utaliacha,kila mwanadamu mwenye akili timamu uwa anapenda kuwa kwenye mahusiano,ingawa kuna watu wengine wana akili timamu na hawako kwenye mahusiano au ndoa kutokana na sababu wanazo zijua wao wenyewe,huendaalikuwa kwenye mahusiano au ndoa na aliumizwa na hataki kusikia swala zima la mahusiano,basi leo nataka nikupe nguzo kuu mbili muhimu ambazo ukizizingatia lazima utaishi katika mahusiano/ndoayako kwa amani  

1:
NGUZO YA KWANZA NI UPENDO
> Upendo siyo neno geni   katika maisha yako,japo uwa unasikia upendo upendo nakupenda nakupenda,je? ni upendo wa dhati kweli toka rohoni ambao mpenzi wako aliyo nao kwako,watu wengi wamekuwa wakitumia neo upendo kama mzaa mzaa vile,ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wengi hawana upendo wa dhati kwa wapenzi wao  toka rohoni,sasa ngoja nikwambie ndugu yangu,ukitaka kuingia kwenye mahusiano/ndoa yako kinacho takiwa utambua kwanza kabla ya yote ni kujua kuwa munapenda kwa dhati,maana upendo ndo kila kitu,hapa ninakupa nguzo mbili lakini ya muhimu kulizo nyingine ni   upendo tu,maana hata kwenye Biblia upendo ndo amri kubwa kuliko zote,maana ukimpenda mpenzi wako kwa dhati lazima mahusiano yenu yatakuwa mahusiano ambayo yako imara maana yanapata baraka toka kwa mwenyezi Mungu maana yeye ndo kaleta upendo huo,kumbuka kuwa hakuna mtu ambae yuko kwenye mahusiano na hataki upendo hayupo na kama yupo basi  akili zake haziko sawa,kila mtu unae muona anaitaji upendo toka kwa mweza wake,na mahusiano mengi yanavunji kwa Mmoja wapo kuto kuwa na upendo kwa mweza wake,kwahiyo ukiwa na upendo kwa mweza wako lazima mahusiano yenu yatakuwa imara hayataweza kuteteleka hata kidogo.

2: NGUZO YA PILI NI KUHESHIMIANA
>Heshima uwa nine dogo sana lakini ndo jambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu yoyote yule,kila jambo unalo taka kufanya katika maisha yako lazima uwe na heshima ya kutosha ndo utaweza kufanikisha jambo hilo pasipo heshima uwezi kufanya jambo na likaenda kama ulivyo tengemea,mfano mzuri vuta taswira kipindi uko shule wanafunzi waliyo kuwa na heshima ndo walikuwa wanafanya vizuri kwenye masomo yako,hapo ndo utajua kumbe heshima ni jambo la muhim katika maisha ya mwanadamu yoyote yule,kwenye maisha ya mahusiano heshima ni jambo la muhimu mno,ndo kama nilivyo kueleza
Pale kwenye nguzo ya kwanza kuwa kila mtu anaitaji upendo wa dhati toka kwa mweza wake hapa pia ndo hvyo hakuna mtu ambae apendi kuheshimiwa na mweza wake,ukizingatia hizi nguzo mbili muhimu lazima utafurahi mahusiano/ndoa yako,maana hizi ndo nguzo muhim za kuimarisha na kujidhatiti katika swala zima la mahusiano.

By Emmanuel mkome (Mr Arsenal)

0767372829

Hakuna maoni