WAFANYAKAZI SAHARA MEDIA WAGOMA KISA HIKI TAPA
Wafanyakazi wa kampuni ya Sahara Media Group Limited inayojumuisha Redio Free Africa,Kiss Fm na Star Tv wamegoma huku wakishinikiza kupewa stahiki zao kadri ya makubaliano waliyoyaweka baina yao na mwajiri wao.
Wakiongea mbele ya ofisi za kampuni hiyo wafanyakazi hao wamelalamikia suala la kucheleweshwa stahiki hizo na wengine kutolipwa kabisa huku mwajiri wao(SMG) akiwakwepa kwa kudai kuwa kampuni hiyo ameshakabidhishwa kwa mtu mwingine.
Aidha wamesema kuwa kucheleweshewa stahiki hizo kwa takribani mwaka na zaidi kunasababisha wafanyakazi hao kushindwa kujikimu kimaisha na familia zao huku wakishindwa kusomesha wanafunzi hivyo kupelekea wengine kupoteza mwelekeo wa maisha.Huku wakiongeza kuwa mwajiri wao amekuwa akiwazungusha na kutowasikiliza jambo ambalo linawaumiza na kuomba serikali iingilie kati suala hilo kwa mwekezaji huyo.
Akijibu tuhuma hizo afisa mwajiri wa kampuni hiyo Bw.Rafael Shilatu amesema kuwa ni kweli wamefika ofisini na mabango lakini wamefanya mkusanyiko usio rasmi hivyo wafanye taratibu kwa kufuata vyombo husika vinavyoshughulikia masuala ya migogoro kati mwajiri na mfanyakazi.
"Ni kweli kuna wafanyakazi na Waliokuwa wafanyakazi ya kampuni yetu ya Sahara ambao wengine walikuwa wanadai stahiki zao lakini wengi wao walikuwa wamesimamishwa kazi na kampuni lakini suala la kuwalipa tutawalipa pole pole kadri siku na kipato kitakavyokuwa kinapatikana na suala la kuwasimamisha tulisimamisha zaidi ya wafanyakazi 150 kutokana na mahitaji ya ofisi "Alisema Shilatu.
Kwa upande wa madai ya kuwa Sahara Media Group LTD imekabidhiwa kwa mtu mwingine Bw.Shilatu amesema kuwa si kweli kuwa kampuni hiyo imekabidhiwa kwa mmiliki mwingine bali bado iko chini ya mmiliki yuleyule na si mwingine.
Hakuna maoni