SI KILA ANAYEKWAMBIA ANAKUOA BASI KWELI NI MUOAJI
SI KILA ANAYEKWAMBIA ANAKUOA BASI KWELI NI MUOAJI
Wanaume wengi siku hizi hutumia kigezo hicho kama sababu ya kuwahadaa wanawake,Unapaswa kuwa makini,Mwanaume akikuambia anakupenda na anataka kukuoa mchunguze kwanza,kabla ya kuruhusu moyo wako kumpenda hakikisha kwanza umejiridhisha huyo anayekwambia anakuhitaji akuoe ni kweli anamaanisha,je ana tabia njema? fanya uchunguzi kwanza,umjue vizuri,ametokea wapi,asili yake ikoje na ikiwezekana familia yake kwa ujumla.
Umjue kama ana hofu ya M ungu,hakuna sababu ya kuharakia ndoa,unaweza kuharakia na mwisho wa siku usidumu.
Unaweza kuingia kwenye ndoa na
jambazi,unaweza kuingia kwenye ndoa na mtu mhuni/katili ambaye yeye muda wote anawaza mambo ya hajabu kama kuua,kuiba,michepuko na mambo mengine ambayo hayampendezi mwenyezi Mungu.
Mtu wa aina hiyo mnaweza kuingia naye kwenye matatizo makubwa sana na ndoa yenyewe ukaiona chungu.
Mchunguze mtu taratibu jipe muda,mshirikishe Mungu katika safari yako,umtambue mwenzi wako ni sahihi au la,ukimtumaini Mungu hakika utapata jibu lililo sahihi,Hakika utampata mwenza ambaye neiyo chaguo lako.
Ipo siku tu,usiumie,usiishi kinyonge,mchunguze mtu kwa mwaka mmoja au hata miwili ndipo ukijiridhisha mpende. By Emmanuel mkome
Maoni/ushauri 0767372829
facebook natumia Emmanuel mkome de Arsenal.
Hakuna maoni