Breaking News

JIFUNZE HAPA KUTUNZA MAHUSIANO YAKO

JIFUNZE HAPA KUTUNZA MAHUSIANO YAKO

Na,Emmanuel mkome

Watu wengi ambao wako kwenye uhusiano wa mapenzi wanalalamika kuwa wenzi wao hawawaoneshi upendo kama ilivyokuwa siku za mwazo za uhusiano wao,wanaona uhusiano wao unalegalega vilevile na mapenzi yanapungua (mithili ya barafu inavyo yeyuka kwenye jua)

ili kuepuka yote hayo,hauna budi kujifunza njia za kuwasha upya moto wa upendo kila wakati kwa kuongeza ukaribu (Intimacy) kati yako na mwenzako.

zifuatazo ni mbinu zitakazokusaidia

1.Msamehe mpenzi wako na kubali kusamehewa naye kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale uhusiano wako,lazima

tujifunze kusamehe umpendae,kutofautiana katika uhusiano kupo sana,na nilazima tuwape nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu,kila hisia za mmoja wetu zina umuhimu,uwezi kujioana vile ulivyo mruhusu mwenzako akwambie yanayomuumiza na msameheme.

2.Linda mwonekano wa mpenzi wako,mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na hukt katika harakati za kutafuta maisha,ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali unalindwa pia,mwonekano wetu lazima uwe halisi na siyo bandia,vile tunavyo viona kwenye tamthiliya na filamu siyo ukaribu ulio halisi,ukianza kupata ukaribu wa kweli
na mpenzi,utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote ,na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao na mpenzi wako tu.

3.Zungumza hisia zako na za mpenzi wako,kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa uhusiano  hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano,lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao,kama vile maisha nk,jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua kuendekea na migogoro isiyosuluhisha husababisha moyo kuwa baridi juu,jiwekeeni muda kila week Aidha mwezi  ili kuzungumza mambo yenu,mwambie umpendae yapi yanakufurahisha kwake na 
yapi yanakuuzi kwake,hii itasaidi kwenye mahusiano wenu kwa hatua kubwa sana.

4.Kutiana moyo na mpenzi wako,kila mmoja awe msaada na tengemeo kwa mwenzake jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo,onyesha heshima katika vitu hivyo pia kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu,mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.

5.Kucheka pamoja na mpenzi wako,kicheko ni mlango wa karibu kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja,kama unaweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza

kupenya katika vyote,usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu,jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.
0767372829

Hakuna maoni