JINSI YA KULAINISHA NGOZI YA MIGUU YAKO
JINSI YA KULAINISHA NGOZI YA MIGUU YAKO
Leo tutaangalia jinsi au namna gani ya kupata ngozi nzuri ya miguu bila ya kwenda kusuguliwa saluni kama wafanyavyo wanawake wengi.
Urembo huu rahisi,tena kwa gharama nafuu unaweza kuupata nyumbani kwako tu na ukaonekana mwenye mvuto zaidi,je? utafanyaje soma hapa:
Urembo huu rahisi,tena kwa gharama nafuu unaweza kuupata nyumbani kwako tu na ukaonekana mwenye mvuto zaidi,je? utafanyaje soma hapa:
LIMAO NA MAFUTA YA MZAITUNI
>>Limao ukichanganya na asali pamoja na mafuta ya mzaituni au ukichukua limao ukachovya kwenye asali na mafuta ya mzaitun4 kisha ukasugua miguu ya utapata majibu mazuri,Baada ya kuisugua acha kwa muda wa dakika 10-20 kisha paka mafuta au losheni unayoitumia.
MAZIWA MGANDO
Maziwa mgando ni mazuri kwa kuondoa sugu kwenye miguu cha kufanya chukua maziwa hayo paka kwenye miguu yako acha kwa muda wa dakika 10-15 kabla ya kuosha,fanya hivyo kila unapokuwa na nafsi utaona jinsi utakavyo kuwa na ngozi laini isiyokuwa na sugu wala haina haja ya kwenda kuoshwa sehemu.
MAFUTA YA NAZI
Chukua mafuta ya nazi paka eneo lililopasuka taratibu fanyia masaji usiku kazi ya mafuta ya nazi ni kulainisha ngozi yako na kuifanya ilainike,ukifanya hivyo utasahau kabisa kwenda kuosha miguu saluni.
usikose makala kama hizi hapa hapa
By EMMANUEL MKOME
0767372829.
0767372829.
Hakuna maoni